Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Mh.Gerson Msigwa, amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza bao moja katika Fainali ya Kombe la Shirikisho ambayo atacheza Simba itakuwa ni Milioni 30.
Simba sc iatcheza michezo miwili ya fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rs Berkane Mei 17 2025 nchini Morocco na marudiano kufanyika Mei 25 2025 jijini Dar es Salaam.
Rais Samia Suluhu Hassan amekua na utaratibu wa kununua kila goli katika michuano ya kimataifa ambayo vilabu vimekua vikishiriki ambapo zawadi hizo zimekua kati ya milioni 5 mpaka 10.
Lakini kutokana na umuhimu wa mchezo huo wa fainali dau hilo limepanda mpaka milioni 30 kwa kila goli ili kuipa Hamasa Simba sc kuelekea mchezo huo.