Home Makala Ihefu Fc Yavunja Unbeaten

Ihefu Fc Yavunja Unbeaten

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Ihefu Fc chini ya Kocha Juma Mwambusi imefanikiwa kuvunja mwiko wa kutofungwa kwa jumla ya mechi 49 za ligi kuu uliowekwa na klabu ya Yanga sc baada ya kuifunga 2-1 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Highlanders ulioko mbalali jijini Mbeya.

Yanga sc ikianza na Fiston Mayele kama mshambuliaji wa kati akisaidiwa na Tuisila Kisinda na Jesus Moloko ilipata bao kipindi cha kwanza kwa kona likifungwa na Yannick Bangala kwa kichwa dakika ya 9 ya mchezo ambapo bao hilo lilirudishwa na Never Tigere dakika ya 39 na mpaka mapumziko matokeo yalikua 1-1.

Ihefu Fc ikiwa na wakongwe Juma Nyoso,Lenny Kissu,Rafael Daud ilitangulia kupata bao la pili kwa kona dakika ya 62 likifungwa na Lenny Kissu baada ya mabeki wa Yanga sc kushindwa kuokoa mpira wa kona bao ambalo lilizua shangwe za kutosha uwanjani hapo.

banner

Yanga sc walijitahidi kushambulia ili kusawazisha lakini mpaka dakika 90 za mchezo matokeo yalikua 2-1 na kuhitimisha rekodi hiyo ya kutofungwa katika michezo 49 ya ligi kuu huku ikifikisha alama 32 za ligi kuu katika michezo 12.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited