Home Soka Israel Aongeza Mkataba Simba Sc

Israel Aongeza Mkataba Simba Sc

by Sports Leo
0 comments

Ikiwa katika maboresho makubwa ya kikosi chake,Klabu ya Simba Sc imefanikiwa kumuongeza mkataba beki Israel Mwenda mpaka mwaka 2026 ambapo amesaini mkataba wa miaka miwili kusalia klabuni hapo.

Simba Sc imeona umuhimu wa kumbakisha beki huyo ambaye mkataba wake wa miaka miwili ulikua unafika tamati Juni 30 mwaka huu ambapo katika dili hilo jipya staa huyo amefanyiwa maboresho katika fedha ya kusaini mkataba (Signing on fees) na mshahara pamoja na bonansi mbalimbali.

Beki amebakishwa kutokana na umuhimu wake kikosini ambapo anaweza kucheza nafasi za beki wa pembeni zote mbili huku akiwa na uwezo wa kutumika kama kiungo wa ulinzi ama winga wa kulia ambapo amekua na kiwango kizuri pamoja na kutopata muda wa kutosha wa kucheza.

banner

Israel alijiunga na Simba sc msimu wa 2021 ambapo mpaka sasa ameitumikia klabu hiyo kwa misimu mitatu akiwa mbadala wa Shomari Kapombe katika eneo la beki wa kulia.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited