Uongozi wa Simba Sc umemtambulisha rasmi ,Charlse Ilanfya kwenye kikosi kinachonolewa na kocha mkuu Sven Vandenbroeck.
Ilanfya alikuwa anakipiga ndani ya KMC ambapo aliibukia huko msimu wa 2018/19 akitokea labu ya Mwadui Fc na amekuwa chaguo la Sven kwa msimu unaoanza wa 2020/2021.
Winga huyo alitupia mabao 6 kati ya 35 ndani ya KMC kwenye ligi iliyomaliza ikiwa nafasi ya 13 katika msimu wa 2019/2020.