Uongozi wa Polisi Tanzania umemalizana na mshambuliaji, Ramadhani Kapera aliyekuwa anakipiga ndani ya KMC.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amesaini kandarasi ya mwaka mmoja Polisi Tanzania akiwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake kuisha ndani ya KMC.
Kapera amesajiliwa ndani ya Polisi Tanzania akiwa ni pendekezo la benchi la ufundi kwani wanaamini atawafaa kuongeza nguvu katika kikosi chao.