Home Makala Job Ajifunga Yanga sc

Job Ajifunga Yanga sc

by Dennis Msotwa
0 comments

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Yanga sc zinasema kuwa mabosi wa klabu hiyo wamefanikiwa kumuongezea mkataba beki wao wa kati Dickson Job kwa miaka miwili zaidi baada ya huu wa sasa kuelekea ukingoni.

Yanga sc ilikua inahaha kumalizana na beki huyo ambaye taarifa zilikua zinadai kua pia ananyemelewa na vilabu vya Simba sc na Azam Fc ambao walikua wamemuandalia donge nono la usajili.

Inasemekana kuwa Job amesaini kwa daul la shilingi milioni sabini za kitanzania huku akipata mshahara wa milioni kumi kwa mwezi katika mkataba huo mpya wa miaka miwili tofauti na dau la mwanzo ambapo Yanga sc walitaka kumpa kiasi cha shilingi milioni sita kama mshahara wa mwezi.

banner

Ilikua ni ngumu kwa Yanga sc kukubali kumuachia beki huyo kutokana na ukweli kwamba amekua na mwendelezo mzuri tangu atue klabuni hapo miaka miwili iliyopita akitokea klabu ya Mtibwa Sugar.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited