Home Soka Kamwe Ashtua Mashabiki Yanga sc

Kamwe Ashtua Mashabiki Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe ametangaza kuachia nafasi hiyo huku akisema muda wake umemalizika ambapo amefanikiwa kuitumikia klabu hiyo kwa miaka miwili tangu alipojiunga akitokea Azam Tv ambapo alikua ni mchambuzi wa masuala ya soka.

Kamwe alitangaza hayo kupitia mtandao wake wa kijamii kuwa anaondoka klabuni hapo ambapo taarifa za ndani zinasema kuwa msemaji huyo tayari amemaliza mkataba wake klabuni hapo huku baadhi ya vipengele vya mkataba mpya vikiwa havijaboreshwa na kuamua bora aondoke.

“Mtumbuizaji mzuri anatakiwa kujua ni wakati gani wa kuondoka Jukwaani. Maneno ya hekima kutoka katika kinywa cha Patrick Loch Otieno Lumumba.

banner

“Na ni Hekima hii, inanituma mbele yenu Wananchi, mashabiki na wanachama wa Klabu yetu pendwa, kuwaambia kuwa, Ni wakati sasa wa kijana wenu kuondoka Jukwaani,” ameandika Kamwe kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram

Hata hivyo taarifa ambazo Sportsleo limezipata ni kuwa tayari mabosi wa klabu ya Yanga sc wamefanikiwa kufanya mazungumzo na staa huyo na tayari atabaki kuendelea na shughuli zake kama kawaida akiwa kama mkuu wa Idara ya Habari ya klabu hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited