Home Makala Katwila Kujinoa Kivingine Mtibwa

Katwila Kujinoa Kivingine Mtibwa

by Dennis Msotwa
0 comments

Kocha mkuu wa Mtibwa Sugar ,Zuberi Katwila ameahidi kurudi kwa kasi na kutoa ushindi wa hali ya juu pindi ligi kuu bara itakaporejea baada ya kusimamishwa na serikali ili kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona.

Katwila alisema kuwa anatafuta mbinu mbadala ya kuitoa Mtibwa katika nafasi ya 14 iliyo na pointi 33 huku ikiwa imecheza mechi 29 pia kuwataka wachezaji wake kuzingatia mazoezi kama walivyokuwa kambini ili kuboresha uwezo wao.

“Ligi ikianza nitarudi kwa kasi kuhakikisha wachezaji wanabadilisha timu irudishe hadhi Morogoro”alisema kocha huyo aliyewahi kuichezea timu hiyo kwa mafanikio makubwa.

banner

Pia Katwila aliwasisitiza wachezaji wake watumie muda huu vizuri  kwa kufuata maelekezo ili waweze kufikia malengo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited