Home Makala Kaze,Hersi Wafuata Mido Rwanda

Kaze,Hersi Wafuata Mido Rwanda

by Sports Leo
0 comments

Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga sc pamoja na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya usajili Eng.Hersi Said wametua nchini Rwanda kumuangalia kiungo matata wa soka Abeid Bigirimana raia wa Burundi anyecheza katika klabu ya Kiyovu Fc.

Inasemekana safari hiyo lengo lake kubwa ni kuangalia maendeleo ya kiungo huyo ambaye ndiye kinara wa mabao Rwanda mpaka sasa, akiwa na mabao (9)  huku pia kuangalia uwezekano wa kufanya nae mazungumzo ya awali endapo wataridhishwa nae kwa ajili ya kumsajili dirisha kubwa la usajili likifunguliwa mwezi juni.

Yanga sc inahitaji mshambuliaji wa kusaidiana na Fiston Kalala Mayele mwenye mabao 11 baada ya Heritier Makambo kushindwa kumpa changamoto staa huyo mkali wa mabao ya kideoni.

banner

Pia kuna nafasi ya kusajili kiungo mshambuliaji wa kigeni baada ya wazawa kama Dickson Ambundo na Farid Mussa kutokua na muendelezo wa viwango vyao huku tayari ikifahamika Hersi alishafanya mazungumzo na kiungo wa Asec Mimosa Ki Aziz kujiunga na Yanga sc.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited