Wachezaji wa timu ya KenGold FC kila mmoja anasafiri kivyake kwenda mkoani Tabora kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya soka ya Nbc nchini dhidi ya Simba Sc utakaofanyika katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Juni 18 2025.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu ni kuwa imeamuliwa wachezaji wa timu hiyo ya wakubwa ambao walikua wametawanyika sasa wanakutana Tabora ambapo kila mchezaji katumiwa nauli asafiri kivyake mpaka mkoani humo.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya vijana KenGold FC na viongozi wameondoka tayari kuelekea mkoani Tabora kwa ajili ya mchezo huo.
Awali timu hiyo ilituma ombi lao la kucheza Dar Es Salaam katika uwanja wa KMC Complex ambalo lilikataliwa na Bodi ya ligi nchini kwa madai limetumwa nje ya muda wa kikakuni.
Tayari klabu hiyo imeshuka daraja na sasa inafanya kukamilisha ratiba ili isipate adhabu ya kufunguwa na shirikisho la soka nchini.