Home Makala Kipa la Kimataifa Laanza kazi Coastal Union

Kipa la Kimataifa Laanza kazi Coastal Union

by Sports Leo
0 comments

Golikipa Ley Matampi  raia wa Congo Drc mwenye umri wa miaka 34 ameanza mazoezi na timu yake mpya ya Coastal Union mara baada ya kuwa ametangazwa kuwa mchezaji mpya wa klabu hiyo yenye maskani yake jijini Tanga.

Matampi ambaye ni golikipa wa zamani wa klabu ya Tp Mazembe na timu ya Taifa ya Congo Drc amejiunga na klabu hiyo dirisha hili la usajili akiwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Fc Lupopo ya nchini Congo Drc.

Kujiunga na kambi ya mazoezi ya klabu hiyo kunatajwa kuwa chachu ya kunyanyua morali ya wachezaji wa klabu hiyo ambao tayari wapo kwenye mazoezi makali chini ya kocha Mwinyi Zahera raia wa Congo Drc na kocha wa zamani wa klabu ya Yanga sc.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited