Bondia Matanzania Hassan Mwakinyo ameelezea masikitiko yake juu ya kipigo cha Tko raundi ya nne kutoka kwa Bondia Mwingereza Liam Smith katika pambano lililofanyika Septemba 4 jijini Liverpool nchini Humo.
Akizungumza na mwandishi Millard Ayo kupitia Kipindi cha Amplifier Mwakinyo amesema kuwa pambano hilo lilikua na nafasi ya kubadilisha sehemu kubwa ya maisha yake kama angeshinda ambapo angevuna pesa ndefu lakini pia angepata pambano jingine lenye pesa ndefu zaidi ambazo zingemtoa katika umaskini.
“Nimekosa hela nyingi sana kutokushinda lile pambano, lakini sijawahi kukata tamaa na silaumu mipango ya Mungu. Ningeweza kuuaga umasikini. Ningeweza kukodisha bodaboda wote wa Tanga, kila mmoja ningempa bajaji tano halafu angekuwa ananirudishia hela kwa namna anayotaka mwenyewe.” ameeleza Hassan Mwakinyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mwakinyo licha ya kupoteza pambano hilo bado ameendelea kushikilia nafasinza juu katika uzani wa kati duniani ambapo barani Afrika akishika nafasi ya pili na nafasi ya sita duniani.