Licha ya kufanya mazungumzo na Simba sc na kuelewena kila kitu kiungo Kelvin Nashon ametua katika klabu ya Singida Big Stars akitokea klabu ya Geita Gold Sc baada ya timu hiyo kununua mkataba wake uliokua umesalia klabuni hapo.
Nashon tayari ameshajiunga na kambi ya klabu yake hiyo mpya iliyoko visiwani Zanzibar katika michuano ya kombe la mapinduzi na alikuwapo katika kikosi cha akiba cha mchezo dhidi ya Azam Fc.
Taarifa zinadai kuwa Singida Big Stars wamekamilisha usajili wa kiungo huyo baada ya kufikia makubaliano na klabu ya Geita Gold sc huku wakitoa dau zuri kushinda lile la Simba sc huku mchezaji nae akipewa dau zuri lililomvutia kujiunga na matajiri hao.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Simba sc ilishafikia makubaliano na mchezaji huyo kuhusu dau la usajili na mshahara huku ilikua imebakiwa na vitu vichache vya kimkataba ili kukamilisha dili hilo.