Home Makala Kmc Yafufuka,Yaichapa Singida Bs

Kmc Yafufuka,Yaichapa Singida Bs

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Kmc imefanikiwa kuchukua alama zote tatu dhidi ya Singida Big Stars katika mchezo wa ligi kuu nchini uliofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Kmc ambayo iko hatarini kushuka daraja sasa inanolewa na kocha Jamhuri Kihwelo “Julio” ambaye alikua kocha wa Namungo Fc siku za hivi karibuni imefanikiwa kushinda mchezo huo na kufikisha alama 29 katika michezo 28 ikisaliwa na michezo miwili.

Mabao ya Kmc katika mchezo huo yalifungwa na Darueshi Saliboko 20′ na Cliff Buyoya 84′ na kuwaacha midomo wazi mastaa kibao waliokua katika kikosi cha Singida Big Star huku kocha Hans Van Pluijm akisema kuwa kufungwa huko ni uzembe wa wachezaji wa kikosi hicho kutotimiza majukumu yao ipasavyo.

banner

“Nimejiandaa vizuru pamoja na vijana na tuna kila sababu ya kushinda mchezo wa leo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutoshuka daraja”Alisema kocha Jamhuri Kihwelo maarufu kama Julio.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited