Home Makala Kocha Azam Fc Achekelea Ushindi Dhidi ya Yanga sc

Kocha Azam Fc Achekelea Ushindi Dhidi ya Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa klabu ya Azam Fc Rachid Taoussi ameendelea kufurahia ushindi wa 1-0 ilioupata klabu yake dhidi ya Klabu ya Yanga sc katika mchezo uliofanyika siku ya Jumamosi iliyopita katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam.

Licha ya kuchukua alama tatu pia ushindi huo umeipandisha Azam Fc mpaka katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu ya Nbc baada ya kufikisha alama 21.

Pia Taoussi anafurahia kuisimamisha rekodi ya Yanga sc ya kutofungwa mchezo wowote katika ligi kuu ya Nbc nchini sambamba na ile ya kutoruhusu bao katika michezo hiyo nane ya ligi kuu huku akiipunguza kasi ya kuelekea kutwaa ubingwa wa ligi kuu mapema.

banner

Kocha huyo alisema kuwa walifanikiwa kuwadhibiti Yanga sc kwa kuwabana wasipate nafasi ya kupiga pasi kama ilivyo kawaida yao.

“Nawashukuru mashabiki wetu kwa kutuunga mkono, tunahitaji zaidi ya hapo kwa sababu sisi ni klabu kubwa. Kuanza kushinda dhidi ya klabu yenye nguvu kama Yanga ni hatua nzuri sana kwetu,” alisema Taoussi aliyechukua nafasi ya Yousouph Dabo klabuni hapo

Akizungumzia maandalizi ya mechi hiyo, alisema walihakikisha wanadhibiti kasi ya washambuliaji wa Yanga kwa kupanga safu ya ulinzi iliyokuwa imara.

“Tulifanya mpango mzuri wa kuweka uwiano kati ya mashambulizi na ulinzi, na hilo liliweza kutusaidia sana.

Hii ni mara ya pili kwa Azam Fc kuiharibia Yanga sc kwa kuifunga katika ligi kuu ambapo pia msimu uliopita walifanya hivyo kwa kuibamiza mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited