Home Makala Ligi kuu Tanzania Bara Septemba

Ligi kuu Tanzania Bara Septemba

by Sports Leo
0 comments

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi kuu Tanzania Almasi Kasongo amesema kuwa ”msimu wa ligi kuu Bara tunatarajia uanze mwezi septemba mwaka huu ingawa mpaka sasa bado hatujapanga tarehe rasmi ya kuanza kwa ligi”.

Hayo yamekuja zikiwa zimepita siku chache tangu kutamatika kwa msimu wa 2020/2021 ambapo klabu ya Simba ilitangazwa na kukabidhiwa ubingwa wa ligi hiyo.Hatua hiyo imeendana pia na kufunguliwa kwa dirisha la usajili kwa wachezaji  wa ndani na wale wa kimataifa kuanzia tarehe 19 mwezi Julai.

Kutangazwa kwa hatua hiyo kunaashiria kuwa timu zitakazo shiriki ligi hiyo msimu ujao zina takribani mwezi mmoja wa kupumzika na kuanza maandalizi ya msimu mpya.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited