Home Makala Maandalizi Uenyeji Afcon 2027 Yashika Kasi

Maandalizi Uenyeji Afcon 2027 Yashika Kasi

by Sports Leo
0 comments

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana mei 29, 2023 ameongoza kikao cha Mawaziri wa nchi za Kenya na Uganda kwa njia ya mtandao ikiwa ni muendelezo wa vikao vya pamoja kwa nchi hizo kuandaa Mashindano ya Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2027, ambacho pia kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Hamis Mwinjuma.

Katika kikao hicho, viongozi hao wameeleza utayari wa wakuu wa nchi hizo na tayari Mashirikisho ya mpira wa Mmguu yote yamewasilisha andiko la kuomba kuandaa mashindano hayo kwa Wakuu hao wa nchi.

Vile vile, kikao hicho kimeazimia kuunda Kamati ambayo itaratibu maandalizi ya awali ya ukaguzi ambao utafanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa ajili ya kuangalia utayari wa nchi hizo kuweza kuandaa Michuano hiyo.

banner

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa wizara Bw. Saidi Yakubu pamoja na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Ndg. Wallace Karia.

Nb:Taarifa na Wizara ya Sanaa,Michezo na Utamaduni.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited