Klabu ya Manchester United imethibitisha kufikia makubaliano na klabu ya Wolves juu ya kumsajili mshambuliaji Matheus Cunha kwa ada ya uhamisho ya pauni Milioni 62.5 ili kujiweka sawa na msimu ujao baada ya kuchemsha msimu huu.
Uhamisho wa mshambuliaji huyo raia wa Brazil unatarajiwa kukamilika rasmi baada ya kukamilika kwa visa yake na usajili baada ya kurejea kutoka kwenye majukumu na timu ya taifa ya Brazil.
Cunha (26) raia wa Brazil amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano na nyongeza ya mwaka mmoja zaidi huku akitarajiwa kuvaa jezi namba 10 iliyokuwa ikivaliwa na Marcus Rashford ambaye anatarajiwa kuondoka klabuni hapo kwenye dirisha la majira ya kiangazi.
Tayari klabu hiyo imetoa taarifa rasmi ya kuhusu kumsajili nyota huyo anayemudu kucheza kama mshambuliaji au kiungo mshambuliaji ambapo taarifa hiyo mesema “Manchester United imefikia makubaliano na Wolves juu ya uhamisho wa Matheus CCunha”,ilisomeka taarifa hiyo
Msimu klabu hiyo imetoka kama katika michuano yote iliyoshiriki huku ikimaliza ligi kuu katika nafasi ya 16 ikiwa ni poromoko kubwa zaidi klabuni hapo katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza.