Kocha wa Simba sc Roberto Oliveira ameonyeshwa kufurahishwa na kiwango cha Aishi Manula tangu ajiunge rasmi na mazoezi ya timu hiyo baada ya kuwa nje kwa takribani miezi sita akijuguza majeraha ya mguu.
Kipa huyo alikua nje ya uwanja baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti nchini Afrika ya kusini mwishoni kabisa mwa msimu uliopita ambapo alipaswa kukaa nje kwa miezi takribani sita.
Baada ya kuwa na kipindi maalumu cha mazoezi binafsi wiki iliyopita staa huyo aliruhusiwa kuanza mazoezi ya pamoja na timu nzima kwa ujumla ambapo mpaka sasa kiasi cha kocha Robertinho kuvutiwa na kiwango cha mchezaji huyo hasa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Dar city na kuamua kumjumuisha katika orodha ya kikosi cha kuwavaa Al Ahly siku ya Ijumaa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Simba sc siku ya ijumaa itakua na mchezo muhimu wa ufunguzi wa michuano ya African Football League ambapo itavaana mabingwa wa bara la Afrika klabu ya Al Ahly katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.