Home Soka Mastaa Yanga Sc Warejea

Mastaa Yanga Sc Warejea

by Dennis Msotwa
0 comments

Baadhi ya Mastaa wa kikosi cha Yanga sc wamerejea nchini kutoka katika majukumu ya timu zao za taifa na kuungana na kikosi hicho mazoezini Avic Town kujiandaa na mchezo wa Derby ya Kariakoo dhidi ya Simba Sc.

Mastaa hao ambao waliondoka kwa muda wa wiki moja kujiunga na kambi za timu zao za Taifa kwa ajili ya michezo mbalimbali ya kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika mwaka 2025.

Stephen Aziz Ki sambamba na Prince Dube jana jioni walikua katika uwanja wa mazoezi kupokea mbinu mbalimbali kwa ajili ya mchezo huo baada ya kuwasili jana mchana.

banner

Khalid Aucho sambamba na Cletous Chama na Kennedy Musonda wanatarajiwa leo kuungana na kikosi hicho mazoezini baada ya kumaliza mechi za kimataifa za nchi zao na walikua wakisubiri kuvunja kambi rasmi kisha kurejea nchini.

Yanga sc itakutana na Simba sc katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Nbc nchini siku ya Jumamosi Oktoba 19 2024 ambapo mchezo huo utakaofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na timu zote kuhitaji alama tatu huku Simba sc ikiwa haijapata ushindi wowote katika michezo mitatu mfululizo baina yao.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited