Home Makala Mauya Ajifunga Miwili Yanga sc

Mauya Ajifunga Miwili Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Kiungo Zawadi Mauya amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia katika klabu ya Yanga sc baada ya ule wa awali kuelekea ukingoni mwishoni mwa msimu huu.

Mchezaji huyo anayecheza eneo la kiungo cha ukabaji amesaini mkataba huo jioni ya leo na kutambulishwa rasmi kupitia mitandao ya kijamii ya klabu hiyo yenye makao yake makuu mitaa ya Twiga na Jangwani kariakoo.

Pia Mauya aliposti picha kupitia mtandao wake wa kijamii wa instagram akisema kwa atakuwepo klabuni hapo kwa miaka mingine miwili zaidi mpaka mwaka 2024.

banner

Mauya anakuwa mchezaji wa tatu kusainishwa mkataba klabuni hapo baada ya Kibwana Shomari na Bakari Nondo Mwamnyeto ambao wote wamesaini mikataba ya miaka miwili miwili.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited