Home Makala Mayele Awasili Nchini

Mayele Awasili Nchini

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Fiston Kalala Mayele amewasili nchini tayari kujiunga na klabu yake ya Yanga sc kufanya maandalizi wa msimu mpya wa ligi nchini ambao utaanza rasmi siku ya August 13.

Mshambuliaji aliyekua kivutio kwa mashabiki wa klabu ya Yanga sc na wadau wa soka nchini msimu uliopita kutokana na kiwango chake kizuri pamoja na aina ya ushangiliaji wake wa kutetema hasa akifunga bao amekua akihusishwa kujiunga na klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika ya kusini pamoja na klabu ya Al Hilal ya nchini Sudan ambayo inatajwa kumuwekea kiasi kikubwa cha fedha.

Kurejea kwa Mayele imekua na habari njema kwa mashabiki wa klabu ya Yanga sc kutokana na umuhimu wake kikosini licha ya kufanya usajili mkubwa eneo la ushambuliaji.

banner

Tayari staa huyo ameungana na wenzake kambini Avic Town iliyopo Kigamboni ambapo anatarajiwa leo kuanza mazoezi na wenzake..

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited