Home Makala Meddie Kagere Awalaza Chali Namungo Fc

Meddie Kagere Awalaza Chali Namungo Fc

by Sports Leo
0 comments

Simba Sc jana ilikuwa  ikicheza na Namungo Fc uwanja wa taifa katika mechi ya michuano ya ligi kuu inayoendelea ambapo Simba wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Namungo Fc.

Bao la kwanza Simba lilipatikana dakika ya 21 kupitia Francis Kahata ambalo lilisawazishwa na Bigirimana Blaise dakika ya 35 kutokea Namungo Fc huku Simba kabla ya kwenda mapumziko waliongeza bao la pili dakika ya 38 kupitia Hassan Dilunga.

Namungo walijipatia bao la pili dakika ya 70 kupitia Lusajo ambaye aliachia shuti kali akiwa nje ya 18 na kumfanya Kakolanya kuambulia kuokota mpira nyavuni.

banner

Meddie Kagere ambaye ni mshambuliaji   wa Simba aliwachapa Namungo bao la tatu dakika ya 88 na kuwafanya walale chali kwani alimaliza shughuli uwanjani kwa kufunga bao la ushindi ambalo limewapa timu yake pointi 3.

Simba inafikisha jumla ya pointi 44 ikiwa nafasi ya kwanza na imefunga jumla ya mabao 38.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited