Uongozi wa Klabu ya Kagera Sugar Umefungua mazungumzo na Kocha wa sasa wa klabu ya Mtibwa Sugar raia wa Marekani Mellis Medo ili kujiunga na klabu hiyo kuchukua nafasi ya kocha Paul Nkata.
Kwasasa kikosi cha Kagera Sugar kipo chini ya kaimu Kocha Bube na hii ni baada ya kufutwa kazi kwa Aliyekuwa Kocha wao Mkuu Paul Nkata na benchi lake lote la Ufundi.
Mazungumzo baina ya Uongozi wa Kocha Mellis Medo na Uongozi wa klabu ya Kagera Sugar Yanaendelea vizuri ambapo siku ya jana kocha Medo aliwaaga wachezaji wa klabu ya Mtibwa Sugar.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Medo anatarajiwa kusafiri kuelekea Kagera siku ya leo ili kumalizana na mabosi wa klabu hiyo na kutangazwa rasmi kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo ambapo atakuja pamoja na benchi lake la ufundi.