Home Makala Messi Aomba Kusitishiwa Mkataba Barcelona

Messi Aomba Kusitishiwa Mkataba Barcelona

by Sports Leo
0 comments

Taarifa zinaeleza kuwa mshambuliaji wa Barcelona,Lionel Messi aliitumia barua klabu yake jana Jumanne, ambapo barua hiyo ilikuwa inaeleza anataka kutumia kifungu kilichopo katika kandarasi yake ili kuweza kuondoka katika klabu hiyo akiwa mchezaji huru mara moja.

Messi amekuwa akidai kuondoka ndani ya Barca takribani siku sita sasa kwani pia alisikika akimpigia kocha mpya wa sasa,Koeman na kumweleza kuwa haoni kama mstakabari wake wa kisoka utaisha vizuri Barcelona hivyo heri akang’oka na kumalizia soka kwingine.

Manchester United na Manchester City wanasemekana kuwania saini ya nyota huyo kwani ni mchezaji bora wa Dunia na endapo atatua katika moja ya timu hizo basi watafika mbali kisoka.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited