Uefa imeahirisha mkutano wake wa kamati ya utendaji uliopangwa kufanyika mwezi Mei 27 kwa sababu ya “nafasi wazi” kuhusu kumbi za mashindano ya mwaka ujao wa Euro 2020.
Uefa imesema mabadiliko ya mkutano huo yamesababishwa na kuwapo kwa idadi ndogo ya maeneo/miji iliyopendekezwa na Uefa ya kuchezewa mashindano ya EURO 2020 mwaka ujao.
Awali mashindano hayo yalipangwa kufanyika katika miji 12 kabla ya kuahirishwa kutoka na janga la Covid-19.
Baraza kuu la soka la Ulaya limetoa taarifa kuwa mkutano huo utafanyika mwezi Juni 17 badala ya Mei 27.