Baada ya kusimamishwa kwa tuhuma za utovu wa nidhamu ndani ya klabu ya Simba sc na kutakiwa kuandika barua ya maelezo kwa Afisa Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba sc Babra Gonzalez bado Benard Morrison hajaandika barua hiyo.
Kwa mujibu wa meneja wa habari na mawasiliano wa klabu hiyo Ahmed Ally ni kwamba mpaka sasa bado mchezaji huyo hajaandika kutoa maelezo kama alivyoelekezwa kufanya na uongozi wa klabu hiyo.
Morrison alijiunga na klabu ya Simba sc baada ya kushinda kesi dhidi ya klabu yake ya zamani ya Yanga sc katika kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji huku Yanga sc waliamua kukimbilia katika mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa michezo (Cas) ambapo mchezaji huyo alishinda.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.