Inaelezwa kuwa nyota wa Yanga, Bernard Morrison anaweza kuonekana akiwa kwenye uzi mweupe na mwekundu kwani tayari amemalizana na uongozi wa Smba hivyo mda wowote anaweza kutangazwa.
Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya GSM ,Hersi Said ambao pia ni wadhamini wa Yanga amesema kuwa inashangaza kwani Morrison bado ana mkataba na kesi yake bado inasikilizwa, hivyo itakuwa ni ajabu kutangazwa kuwa ni mchezaji wa simba wakati kamati inafuatilia mambo yaliyopo.
“Ni muda mrefu viongozi wa Simba wamekuwa wakimlaghai ili kumpa mkataba hivyo kama atatangazwa kuwa ni mchezaji rasmi wa Simba Sc basi itatoa picha kwamba Simba walikuwa nyuma katika haya,” amesema Hersi Said
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.