Home Soka Morrison Aungana na Mashujaa Fc

Morrison Aungana na Mashujaa Fc

by Dennis Msotwa
0 comments

Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Simba sc na Yanga sc Benard Morrison amejiunga na klabu ya mashujaa Fc ambayo ipo jijini Dar es salaam kwa mazoezi ya gym akijiweka fiti baada ya kupona majeraha yake yaliyomfanya akae nje kwa takribani miezi sita akiugulia.

Mchezaji huyo mwenye vituko alijiunga na klabu ya Far Rabat iliyokua chini ya kocha Nasreddine Nabi lakini aliumia vibaya hali iliyomlazimu kukaa nje ya uwanja kwa miezi hiyo sita ambapo alikuja nchini kwa ajili ya kujiuguza majeraha yake hayo mpaka sasa amepona.

Awali staa huyo alijichimbia Avic Town akifanya mazoezi kisha baadae aliamua kuondoka kurudi kwao nchini Ghana na kisha amerejea tena nchini ambapo mpaka sasa licha ya kupona bado hana timu akiwa ni mchezaji huru.

banner

Pamoja na kuwa na kipaji halisi cha soka mchezaji huyo kwa asilimia kubwa kipaji chake kinaathiriwa na kukosekana kwa nidhamu na bidii ya mazoezi ambapo ana mambo mengi ya nje ya uwanja na ndio sababu kubwa inayomfanya mara kadhaa akose timu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited