Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Benard Morrison amefungiwa mechi tatu mfululizo na kamati ya usimamizi wa ligi kuu nchini kwa kosa la kumkanyaga mchezaji Lusajo Mwaikenda katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc uliomalizika kwa sare ya 2-2.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka bodi ya ligi kuu nchini adhabu hiyo imetolewa na bodi ya ligi kuu nchini kwa uzingativu wa kanuni ya 42:5(5.6) ya ligi kuu kuhusu udhibiti wa wachezaji.
Morrison kutokana na adhabu hiyo ataikosa michezo mitatu dhidi ya Namungo Fc,Ruvu Shooting Fc na dhidi ya mahasimu wao wakubwa Simba sc mchezo ambao mashabiki wa klabu ya Yanga sc wangependa ashiriki ili kuwalipiza kisasi watani hao wa jadi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Hii si mara ya kwanza kwa Morrison kufungiwa kwani imekua ni kawaida kwake kutokana na kuwa na utovu wa nidhamu huku pia akikabiliwa na matukio tata kiwanjani mara nyingi.