Home Makala Mourinho Awasaidia Wazee Wa Karantini

Mourinho Awasaidia Wazee Wa Karantini

by Sports Leo
0 comments

Kocha mkuu wa Tottenham,Jose Mourinho ametoa msaada wa chakula kwa wazee wa kituo cha Your Door Step kilichopo Enfield.

 

Mourinho aliwatembelea watu wa kituo hicho kilicho karibu na sehemu ya kufanyia mazoezi ya timu yake ya Spurs ambapo aliwapelekea chakula na vitu  muhimu ikiwa ni sehemu ya msaada kwa jamii inayomzunguka.

Wazee hao walishauriwa kukaa karantini kwa muda wa wiki 12 ili kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona ambayo kwa sasa yameshaenea takribani dunia nzima.

banner

“Nipo hapa kwenye kituo cha Love Your Door Step Enfield kwa ajili ya kuchangia kile ambacho ninacho ambacho ni chakula na unaweza kujitoa pia kwa ajili ya kuwapa msaada iwe ni chakula, fedha ama kujitoa kwa ajili yao,” amesema kupitia video iliyotumwa na Love Your DoorStep kwenye akaunti ya Twitter.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited