Home Makala Mpole Arejea Fc Lupopo

Mpole Arejea Fc Lupopo

by Sports Leo
0 comments

Licha ya kutawala kwa tetesi kuwa mshambuliaji George Mpole yupo njiani kujiunga na klabu ya Yanga sc tayari mchezaji huyo amejiunga na klabu yake ya Fc Lupopo ya nchini Congo Drc kujiandaa na maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu.

Mople ambaye hakupata nafasi ya kuichezea timu hiyo msimu uliopita kutokana na kukosa nafasi katika usajili wa kucheza michuano ya Caf baada ya jina lake kuonekana katika usajili wa Geita Gold Fc huku pia ligi kuu ya nchi hiyo ilisimamishwa na kufutwa kutokana na vita iliyokua ikiendelea nchini humo hivyo kumfanya arejee nchini bila kutumika na klabu hiyo mpya.

“Msimu uliopita kwangu ulikuwa na changamoto mbili ya kwanza nisingeweza kucheza michuano ya CAF kwa sababu tayari nilicheza nikiwa na Geita Gold, jambo la pili ligi ikafutwa hivyo nikajikuta sijafanya kile nilichokitarajia.

“Najua kikosi chetu kina ushindani, pia wanasubiri kwa hamu kuona nitafanya nini, maana wakati natambulishwa kwa mara ya kwanza wachezaji wenzangu walifurahia kutokana na rekodi ya mabao 17 niliyoyafunga Geita.”Alisema Mpole

Mpole kwa sasa yupo nchini Congo Drc akijiandaa na msimu mpya kuonyesha uwezo wake tangu alipotwaa tuzo ya mchezaji bora hapa nchini Tanzania msimu wa ligi kuu ya Nbc wa 2021/2022.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited