Home Makala Mpole Atwaa Kiatu cha Dhahabu

Mpole Atwaa Kiatu cha Dhahabu

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa klabu ya Geita Gold Fc George Mpole ametwaa tuzo ya mfungaji bora wa ligi kuu nchini baada ya kufunga bao 1 katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union na kutimiza jumla ya mabao 17 akimzidi Fiston Kalala Mayele wa Yanga sc mwenye mabao 16.

Mpole kabala ya michezo ya mwisho ya ligi kuu nchini alikua ana magoli 16 sambamba na Mayele lakini katika mchezo huo dhidi ya Wagosi wa kaya Mpole alifunga bao moja huku Mayele akishindwa kufunga katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam na kumfanya Mpole kuwa kileleni kwa goli moja zaidi dhidi ya 16 za Mayele.

Takimu za mwisho zinaonyesha kuwa Mpole amefunga mabao 17 akiwa na assisti 4 katika mechi 30 ambazo alicheza jumla ya dakika 2427 huku Fiston Mayele akiwa na mabao 16 na assisti 5 katika michezo 30 ambayo alicheza jumla ya dakika 2373 huku Reliants Lusajo akiwa katika nafasi ya tatu na magoli 10.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited