Home Makala Mshambuliaji Simba Aomba Namba Yanga

Mshambuliaji Simba Aomba Namba Yanga

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji  wa zamani wa Simba mwenye asili ya Urundi, Laudit Mavugo amesema kuwa anatamani kuona anarejea kuchezea timu kubwa tena nchini Tanzania ikiwemo Yanga kwani lengo lake ni kutaka kuthibitisha ubora wake.
Mavugo kwa sasa anakipiga katika klabu ya Napsa Stars ya Zambia ambapo katika msimu uliopita alifanikiwa kuibuka mfungaji bora licha kwa msimu miwili aliyocheza Simba hakufanikiwa kuonyesha bora wake kwenye eneo la ufungaji.
“Unajua timu kubwa kwa Tanzania zinajulikana kama vile Yanga au Azam Fc hivyo nadhani itakuwa sawa kwangu kuweza kuthibitisha kile ambacho kilionekana kuwa kipo tofauti wakati nacheza Simba sasa kama ikitokea ofa nitakubali kuja hata kama ni Yanga,” alisema Mavugo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited