Straika wa klabu ya Simba sc Chrispine Mugalu ameonekana kuwa fiti kuivaa timu ya Yanga sc katika mchezo wa ligi kuu baada ya jana kuingia uwanja kuivaa Kagera Sugar.
Awali kocha Sven Vandebroek alikaririwa akisema kuwa washambuliaji wake Mugalu na Meddie Kagere kuwa majeruhi hivyo wanaweza kutoshiriki mchezo huo wenye hamasa zaidi nchini.
Lakini jana staa huyo alionekana kuwa fiti akikabiliana na mikiki ya mabeki Ally Sonso na wenzake japo hakufanikiwa kufunga bao lolote.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.