Klabu ya Simba sc imekamilisha usajili wa kiungo Mshambuliaji Ahoua Jean Charles kutokea klabu ya Stella Club Abijani ya nchini Ivory Coast kwa mkataba wa miaka miwili kuja kurejesha ufalme uliopotea Msimbazi kwa muda wa miaka mitatu sasa.
Kiungo huyo ndie mchezaji bora wa ligi kuu ya nchini Ivory Coast kwa msimu huu akifanikiwa kufunga mabao 12 na kutoa pasi za mabao 9 na kufanya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora kwa msimu huu ulioisha nchini humo huku pia akizikaa ofa nyingi za Afrika Magharibi ambapo timu kadhaa zilikua zinamtolea macho.
Kiungo huyo anakuja kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Cletous Chama ambaye amejiunga na Yanga sc kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwingine licha ya jitihada za makusudi za mabosi wa klabu hiyo kumuongezea mkataba wa kusalia klabuni hapo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mpaka sasa Simba sc imewasijili Lameck Lawi,Stephen Mukwala na Joshua Mutale huku ikiwaongezea mikataba mastaa Kibu Dennis,Mzamiru Yassin na Israel Mwenda kuendelea kusalia klabuni hapo.