Kiungo mkabaji aliyemaliza mkataba wake katika klabu ya Simba Sc Fabrice Ngoma (31) anakaribia kujiunga na klabu ya Hassania d’Agadir kutoka Morocco muda wowote kuanzia sasa.
Kiungo huyo mwenye uwezo wa kucheza katika eneo la ulinzi na ushambuliaji anaondoka nchini muda wowote kwenda nchini humo kukamilisha dili hilo la usajili ambapo atavuna pesa ndefu.
Ngoma ambaye usajili wake ulivuma hapa nchini akihusishwa zaidi na Yanga sc kisha akatua Simba Sc ambayo ameitumikia kwa miaka miwili mfululizo mpaka msimu huu.
Dili hilo litakamilika kwa urahisi zaidi kwa sababu kwa sasa kiungo huyo ni mchezaji huru mara baada ya mkataba wake kutamatika Simba Sc na mabosi wa klabu hiyo hawajaonyesha nia ya kumuongezea ikitajwa kuna ni kinara wa misimamo hasa kuhusu kudai posho na malipo mengine klabuni hapo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Tayari kiungo huyo ameshaaga klabuni hapo kupitia mitandao yake ya kijamii akiwaaga mashabiki na wachezaji wenzake akiwatakia kila la kheri.