Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Pacome Zouzoua anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa takribani siku kumi akiuguza majeraha ya enka aliyoyapata katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Klabu ya Azam Fc April 10 2025.
Pacome aliumia punde baada ya kufunga bao la kwanza kwa klabu yake na sasa anapaswa kuwa nje kwa siku hizo mpaka atakapopona kabisa.
Jeraha hilo linasemekana kuwa sio geni kwa staa huyo kwani pia aliwahi kuumia kuelekea mchezo wa klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Usm Algers ambao Yanga sc walishindwa kufuzu hatua ya robo fainali baada ya kutoka suluhu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Hata hivyo taarifa njema ni kuwa staa huyo ataiwahi baadhi ya michezo ya ligi kuu na kombe la Shirikisho la Crdb kutokana na michezo hiyo kuwa mbalimbali na hivyo kama atapona kwa wakati basi moja kwa moja ataiwahi.
Msimu Pacome amekua katika kiwango bora mpaka sasa akichangia upatikanaji wa mabao 18 katika kikosi hicho nyuma ya Prince Dube aliyechangia upatikanaji wa mabao 20 mpaka sasa.