Home Makala Pacome,Ki Hatihati Yanga sc

Pacome,Ki Hatihati Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Viungo washambuliaji wa klabu ya Yanga sc Stephane  Azizi Ki na Pacome Zouzoua wamezua hofu kuelekea mchezo dhidi ya Simba kutokana na majeraha ambayo waliyapata katika mchezo uliopita dhidi ya Singida Fountain Gate Fc.

Baada ya mchezo huo kumalizika mastaa hao wote wawili walionekana wakitoka uwanjani wakiwa wanachechemea na kuzua hofu kuhusu kuwepo katika mchezo wa Novemba 5 dhidi ya Simba sc utakaofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mastaa hao kwa pamoja wamefunga jumla ya magoli tisa ya ligi kuu ambapo Ki amefunga mabao sita na Pacome akifunga mabao matatu wakitengeneza safu ngumu ya ushambuliaji ya Yanga sc ambapo viungo hao wamekua moto wakishirikiana na Maxi Nzengeli.

banner

Mpaka sasa bado haijajulikana ukubwa wa majeraha ya viungo hao wanaotegemewa katika kikosi hicho ambapo ripoti ya daktari wa klabu hiyo Moses Etutu ndio itaamua kuhusu uwepo wa mastaa hao kikosini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited