Klabu ya Pamba Jiji iliyopanda ligi kuu kuanzia msimu ujao imefanya maamuzi magumu ya kuachana na wachezaji wote sambamba na benchi la ufundi ambao wameipandisha timu hiyo katika ligi kuu kutoka katika ligi daraja la kwanza (Championship).
Katika Taarifa iliyotolewa kwa umma inasema kwamba klabu hiyo imeachana na wachezaji sambamba na benchi la ufundi baada ya mikataba yao kufika mwisho na sasa itaanza upya zoezi la usajili wa benchi la ufundi pamoja na wachezaji wapya ambapo tayari imemalizana na kocha Goran Kuponovic aliyekua Tabora United.
“Tunapenda kuwajulisha wapenzi wa Pamba Jiji na wadau wa soka kuwa benchi la ufundi pamoja na wachezaji walioipandisha timu yetu Ligi Kuu Bara wote wamemaliza mikataba yao.”Ilisomeka taarifa hiyo
Hata hivyo pia kwa upande wa wachezaji ambao waliipandisha timu hiyo baadhi wameanza kusajiliwa kwa kupewa mikataba mipya akiwemo kipa Shaban Kado,Haruna Chanongo na Joram Gustavo ambao tayari wamelipwa pesa zao za usajili kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa klabu hiyo ina mpango wa kuwabakisha wachezaji takribani kumi walioipandisha timu hiyo daraja na tayari baadhi wameanza kulipwa fedha za mikataba mipya ambapo wataungana na mastaa wapya watakaosajiliwa tayari kupambania nembo ya klabu hiyo.