Klabu ya soka ya Pamba Jiji Fc yenye makao yake makuu Jijini Mwanza imeamua kuwaomba wachezaji wawili wa klabu za Simba Sc na Yanga Sc Jonathan Ikangalombo na Augustine Okejepha kwa mkopo baada ya kukosa nafasi katika timu hizo kiasi cha kuelekea kuvunjiwa mikataba yao.
Tayari klabu ya Simba Sc yenyewe imefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Okejepha kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake huku Yanga Sc nao mpaka sasa wapo katika mazungumzo ya kuvunja mkataba wa Jonathan Ikangalombo ama kumtoa kwa mkopo jambo ambalo mshambuliaji huyo amegoma.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh.Said Mtanda ambaye ni mlezi wa Pamba Jiji amesema kuwa wapo kwenye mazungumzo kwa ajili ya kuwasajili kwa mkopo mastaa hao kutoka katika timu hizo.
“Tumewaandikia barua Yanga kumuomba Jonathan Ikangalombo kwa sababu tunao uwezo wa kumchukua na kumpa anachokitaka. Pamba Jiji FC sio wanyonge, wala hatuna tatizo lolote,Tumewaambia Simba kama Okejepha mmemtoa sisi [Pamba Jiji FC] tunamtaka.Mleteni tutamlipa tutafanya nae kazi”.Alisema Mh.Mtanda
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Pamba Jiji Fc ipo kwenye maboresho makubwa ya kikosi chake ambapo imemuajiri kocha Francis Baraza kuchukua nafasi ya Fred Felix Minziro huku ikianza kusajili mastaa wa maana kwa ajili ya msimu ujao.