Klabu ya Simba Sc imempa mapendekezo ya mkataba kiungo wa klabu ya Kmc Ahmed Pipino ili aupitie na kufanya maamuzi ili klabu hiyo iangalie uwezekano wa kufungua mazungumzo ya kumsajili katika klabu yake ya Kmc aje kuungana na mastaa wa klabu hiyo kwa ajili ya msimu ujao.
Taarifa za ndani zinasema kuwa kiungo huyo meshasema ndio kujiunga na Simba Sc na Kmc Fc wamekubali ofa ya Simba Sc na wapo tayari kumuuza kiungo huyo na kilichobaki ni maslahi binafsi ya mchezaji huyo na klabu ya Simba Sc jambo ambalo linaweza kumalizika muda wowote.
Hata hivyo Simba sc inapaswa kuwa na subira kutokana na kiungo huyo kuwa katika kambi ya timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambayo inashiriki michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) ambapo inaongoza kundi B la michuano hiyo ikiwa na alama tisa.
Pipino tayari ameshapitishwa na kocha Fadlu Davis ambaye ameridhishwa na uwezo wa kiungo huyo na anamuona anaweza kufaa katika mfumo wake kikosini humo ikizingatiwa kuwa mchezaji huyo ni mzawa na atachukua nafasi ya kiungo Omary Abdallah Omary ambaye amerudi katika klabu ya Mashujaa Fc.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kiungo huyo hataweza kujiunga na kambi ya Simba Sc inayoendelea nchini Misri ambapo endapo dili hilo litakamilika atajiunga na klabu yake hiyo mpya mwanzoni mwa msimu katika michuano ya ngao ya jamii inayotarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.
Msimu huu usajili wa klabu ya Simba Sc upo chini ya kocha Fadlu Davis ambaye amekua na mamlaka ya mwisho kiufundi kuamua aina ya usajili wa mchezaji anayetakiwa klabuni hapo na ndio chanzo kikubwa cha kumkataa beki wa Coastal union Miraji Abdalah Zambo na kumsajili beki Anthony Mligo kutoka Namungo Fc.