Home Makala Rasmi Pamba Jiji Fc Yaishusha Daraja Kagera Sugar Fc

Rasmi Pamba Jiji Fc Yaishusha Daraja Kagera Sugar Fc

by Sports Leo
0 comments

Sasa ni rasmi klabu ya soka ya Kagera Sugar Fc imeshuka daraja mpaka ligi daraja la kwanza kwa msimu ujao baada ya klabu ya Kengold Fc kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Pamba Jiji Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini uliofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Kagera Sugar imeshuka rasmi daraja hadi ligi daraja la kwanza (Championship) baada ya leo Pamba jiji Fc kushinda mabao 2-0 dhidi ya KenGold Fc na kufikisha alama 30 ambazo zimewafanya kuwa salama salimini.

Pamba Jiji Fc baada ya ushindi huo sasa wamesaliwa na michezo miwili iliyowafanya kuwa salama huku Kagera Sugar Fc wakibaki katika nafasi ya 15 ya msimamo wa ligi kuu ya Nbc wakiwa na alama 22 ambapo hata wakishinda michezo miwili iliyobaki bado watabaki katika nafasi hiyo hiyo.

banner

Mabao ya Pamba Jiji Fc katika mchezo wa leo yalifungwa na Yonta Camara dakika za 30 na 60 na kuizima Kagera Sugar moja kwa moja.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited