Home Makala Samia Anunua Mabao Simba sc,Yanga sc

Samia Anunua Mabao Simba sc,Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu ametangaza kununua kwa Sh5 milioni kila bao litakalofungwa na Simba na Yanga katika michezo yao ya kimataifa ya mwisho wa wiki hii.

Hayo yamebainishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa leo hii huku timu hizo zikiwa na kibarua kwa mechi ya pili hatua ya makundi baada ya mechi za kwanza kufungwa ugenini.

Simba itacheza Jumamosi dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika saa 1:00 usiku uwanja wa Mkapa na Yanga sc itaikaribisha TP Mazembe Jumapili saa 1:00 usiku katika mechi ya Kombe la Shirikisho zote zikiwa ni mechi za pili kwa kila timu.

banner

Simba sc na Yanga sc zinapaswa kuhakikisha zinafuzu hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika kwa Simba sc na Yanga sc katika michuano ya kombe la shirikisho ambapo ushindi wa michezo ya nyumbani ni muhimu ili kufuzu hatua ya robo fainali kwani kupata alama tatu ugenini ni mtihani.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited