Nahodha msaidizi wa Yanga,Juma Abdul amesema kuwa mdhamini wao GSM amewaongezea nguvu ya kufanya mazoezi wakiwa nyumbani kutokana na kupewa fursa ya kufanya manunuzi kwenye duka la michezo lililopo Mlimani City.
Abdul amesema kuwa vifaa hivyo walivyonunua vitawasaidia kufanya mazoezi nyumbani kwa umakini huku wakichukua tahadhari dhidi ya COVID-19 ambavyo ni virusi vya Corona.
“Fursa ya kufanya manunuzi kwenye duka la mdhamini wetu tumeifurahia na imetufanya tuwe na furaha zaidi kwani itatufanya tuendelee kufanya mazoezi nyumbani na kuendelea kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona,” alisema nahodha huyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.