Klabu ya Simba Sc itazindua jezi maalumu kwa ajili ya michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho barani Afrika siku ya Jumatano mchana katika ofisi za mdhamini wa jezi hizo Sandaland the only one Kariakoo Jijini Dar es Salaam.
Jezi hizo zinatarajiwa kuwa chache huku zitaizwa kwa bei ya rejareja moja kwa moja ili kuhakikisha hakuna walanguzi.
Simba sc inatarajiwa kuanza kampeni ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Onze de Marquiz ya nchini Msumbiji katika mchezo utakaofanyika Novemba 26 jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.