Klabu ya Simba Sc imepoteza mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Al Masry katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Suez Canal nchini Misri.
Simba sc ilijikuta ikikubali mabao mepesi licha ya kucheza mechi hiyo vizuri kwa dakika zote tisini ambapo walikua wanaongoza kwa kumiliki mpira na kutengeneza nafasi za kufunga.
Simba sc iliyomkosa beki wake Che Malone Fondoh ilitanguliwa kufungwa kwa shuti kali la Abderahim Deughemom dakika ya 16 lililomshinda kipa Moussa Camara kutokana na mpira kudunda.
Bao hilo lilidumu mpaka kipindi cha pili ambapo pia simba sc walikosa nafasi kadhaa kupitia kwa Lionel Ateba na Kibu Dennis.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kipindi cha pili Al Masry waliendelea kushambulia kwa kushtukiza huku wakiubana uwanja na kufanikiwa kuwadhibiti Simba sc ambao walikua wanacheza kwa maelewano na kushambulia kwa kasi.
Teknolojia ya mwamuzi wa njia ya video iliwafaidisha Al Masry baada ya mwamuzi kuwapa bao la pili ambalo awali ilidhaniwa kuwa ni mfungaji ameotea ambapo mpira uliopanguliwa na Moussa Camara ulimgonga Mshambuliaji wa Al Masry John Okoye na kuwapa wenyeji bao la pili.
Mpaka dakika 90 zinamalizika Simba sc walikubali kichapo hicho na sasa wana kazi kubwa ya kufanya April 9 2025 watakapovaana na timu hiyo katika mchezo wa marudiano.