Klabu ya Simba Sc Yapotezea Mkutano na Wanahabari ambapo haijatuma wawakilishi kwenye mkutano wa waandishi wa Habari kuelekea mchezo wake dhidi ya Yanga sc kuzungumzia maandalizi yake ya mchezo huo unaotarajiwa kupigwa kesho Juni 25, 2025 saa 11:00 jioni kwenye Dimba la Benjamin Mkapa.
Kwa mujibu wa kanuni ni kuwa siku moja kabla ya mchezo wa ligi kuu ya Nb nchini timu zitakazo kutana kiwanjani kutuma kocha pamoja na nahodha kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari kuelezea juu ya maandalizi ya mchezo husika.
Leo Simba sc haikutuma mwakilishi yeyote licha ya juhudi za maafisa wa bodi ya ligi kuwatafuta kwa ajili ya tukio hilo.
Taratibu za Ligi hiyo ni kuwa siku moja kabla ya mchezo, timu husika zinatakiwa kutuma Kocha na Mchezaji kuzungumza na Wanahabari kuhusu mchezo unaofuata ambapo ni ratiba pia inayofuatwa na Azam TV ambao wanahusika kurusha matangazo ya Ligi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kutokana na kukiuka kanuni hiyo sasa klabu hiyo itapigwa faini kama kanuni inavyosema.