Home Makala Simba Sc Yarejea Kileleni Nbc

Simba Sc Yarejea Kileleni Nbc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba Sc imefanikiwa kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini baada ya kuifunga timu ya Tabora United kwa mabao 3-0 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

Simba sc ikicheza mbele ya maelfu ya mashabiki waliofurika nchini ilipata bao la kwanza mapema dakika ya 12 likifungwa na Lionel Ateba kwa shuti kali baada ya mabeki kuzubaa kumkaba Ellie Mpanzu aliyempa pasi nzuri mfungaji.

banner

Tabora United hawakua na siku nzuri kazini kwa pamoja na kujitahidi kusawazisha walijikuta wakifungwa bao la pili na Ateba dakika ya 34 ya mchezo kwa penati baada ya Ellie Mpanzu kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari akielekea kufunga.

Simba sc baada ya mabao hayo iliuchukua mchezo na kucheza soka safu mbele ya utitiri wa viungo wa Tabora United na kufanikiwa kupata bao la tatu likifungwa na Shomari Kapombe dakika ya 66 ya mchezo.

Tabora United waliathirika na kukosekana kwa Heritier Makambo na Yacouba Songne kwa muda mwingi walishindwa kupeleka mashambulizi kwa usahihi golini.

Simba sc sasa imefikisha alama 43 kileleni mwa msimamo ikicheza michezo 16 huku Tabora United wakiwa katika nafasi ya tano msimamo na alama 25.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited