Benard Morrison alitosha kabisa kuipa timu yake ya Yanga ushindi muhimu dhidi ya watani wao wa jadi Simba Sc siku ya jana ,Uwanja wa Taifa licha ya kufanyiwa faulo nyingi kutoka kwa wachezaji wa Simba.
Nyota huyo wa Yanga aliwainua mashabiki dakika ya 44 kwa kupiga mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja nyavuni na kumshinda nguvu mlinda mlango wa Simba Aishi Manula .
Furaha waliyoipata mashabiki wa Yanga kwa kutangulia kuifunga Simba bao la kwanza la pekee lililodumu dakika 90 za mchezo ziliinua mkono wa kulia wa Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli aliyehudhuria mechi hiyo akiwa amevaa jezi ya mkono wa kulia yanga na kushoto Simba.
Pia Raisi wa CAF ,Ahmed Ahmed hakuwa nyuma kushuhudia matokeo hayo ambayo yameirudisha yanga ya zamani katika mstari sahihi chini ya kocha wao mkuu Luc Eymael ambayo tangu 2016 yanga haikuwa kuishinda Simba.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Ushindi huo unaifikisha Yanga nafasi ya tatu ikiwa na pointi 50 katika mechi 25 alizocheza huku Simba ikibaki kileleni kwa pointi 68 katika mechi 27 alizocheza.